Story: BATA MREFU 3
Writter: ALNORD SPORTIEVE
Contact: 0655415200
ILIPOISHIA SEHEM YA 2
Walipita chalinze,morogoro,kibaha hatimaye wakaingia UBUNGO
BUS TERMINAL ambapo ALNORD ndio alichanganyikiwa kabisa
kwani aliyaona majengo makubwa(maghorofa) ambayo alikua
akiyaona kwenye TV tu kule kijijini kwao kwenye mabanda ya
video...
Alihamaki sana had ilibak kidogo agongwe na gari pind
walivokua wanavuka barabara ndipo CHUMA akaona ni bora
achukue tax maana hali ile ilionyesha wazi kabisa kua angeweza
kupata aibu mjini pale...ndani ya lisaa limoja na nusu walifika
nyumban kwa baba ake mkubwa(MR. ABDALLAH
CHUMA)...ambapo alipokelewa kwa furaha sana...na wakampa
mizigo HOUSE GIRL wa pale nyumban...nae akaketi seblen
akisubiri nin kinafuata
ENDELEA
...Alnord alikua akiangaza macho huku na kule ndan ya nyumba ile ambayo kiukwel ilikua ni ya kifahari...hakuweza kufikiria kua atakuja kuiona nyumba nzuri kama ile...sio siri alizubaa kiac kwamba hata kaka yake alivokuja kumuita pale seblen ili akamuoneshe chumba atakachokua analala hakuweza kumsikia had alivompiga begani ndipo akashtuka...
"Dogo mbona umezubaa hivo ndugu yangu? Twende nkakuonyeshe chumba chako kule" alisema CHUMA baada ya kumshtua ALNORD ambae mawazo yake yalimpeleza had akahisi yupo kule kwa obama anaishi maisha ya kizungu baada ya kuona furniture nzuri sana na zilizoonekana ni za gharama...
"Ha..ha..hapana kaka nilikua nakumbuka safari yetu ilivokua ndefu...ila sio siri nyumba yenu ni nzuri sana...yani mi nilidhan na huku nyumba zote ni za udongo kama kijijin kwetu". Alizuga vile ALNORD huku akiinuka na kumfuata kaka ake ambae alikua ametangulia mbele kidogo...mpaka walipofika kwenye chumba kimoja ambacho kilikua ni self contained...yan choo na bafu ndani,TV na makolobwezo kibao...kilikua ni kizuri sana kwan pia kilikua na sofa set moja ya kawaida..
"Yeleuwiiiiii....hasa kaka umenleta chumban kwa baba mkumbwa kufanya nin?" Aliuliza kijana yule ambae alikua ni mshamba kupita kiasi..
"Aaaaah dogo acha masihara...hik ndio chumba chako,halafu mlango ule pale ni choo,na bafu ipo mulemule...vyote unavyoviona katika chumba hiki kua huru kukitumia na usisite kuniambia ukiwa na tatizo lolote..sawa dogo? Sasa nenda ukaoge halafu uje sebleni tule" aliongea CHUMA huku akiwa amemaliza kumuonyesha kila kitu kilichopo chumbani kule na yeye kuondoka akimuacha ALNORD mule ndan...
ALNORD hakujibu chochote zaid ya kujitupa kwenye gule gukitanda gwenye vipimo vya sita kwa sita...akiwa haamin kua atakua analala kwenye godoro tofaut na kule kijijin kwao ambako alikua analala kwenye mkeka...
Alivua nguo zake kisha akaenda bafuni kule ambako alikuta taulo jeupeeeee,sabuni ya dettol active,sink Kubwaaa ambalo kwa yeye alihisi wenda litakua bwawa lililokauka maji,na kwa pemben juu aliona bomba la mvua na koki chin yake...ambayo haikumpa tabu kujua pale panafungua maji kwan hata kijijin kwao kulikua na bomba moja la kijiji..hivo alifungua na kushangaa maji yanatoka kwa juu alimanusura akimbie ila alijikaza na kuanza kujipaka sabuni ile ambayo harufu yake ilimvutia mnooo...kisha akajisafisha mapovu na kujipukuta na taulo akatoka zake...
Hakujua apake yapi na aache yapi maana alikutana na mafuta ya aina nyingi kwenye dressing table ya chumban kwake...akaamua kuchukua kopo moja lililoandika VASELINE MEN na akajipaka,akabadili nguo zake na kuvaa nguo alizozikuta kitandan kwake na kujua kua kaka yake ndie aliemletea..kiukwel nguo zilipendeza sana mwilin mwa ALNORD hasa ukuzingatia alikua na sura nzuri,pia t-shirt ilimbana na kuonesha kifua chake kilichojaa vizur...
Basi akatoka zake na kuelekea seblen...kwa bahat mbaya kutokana na wingi wa milango ya vyumba na ugeni wake akajikuta badala ya kuingia mlango wa seblen aliingia kwenye chumba cha HOUSE GIRL ambae alikua mtupu kama alivozaliwa kwan alikua ametoka kuoga...
*******
Baba yake alimuandalia kila kilicho cha muhimu katika safari yake ambako alikua anaenda kukaa peke yake(kujitegemea)...aliviandaa kwa siri kwani aliogopa kama mke wake angeviona ingekua balaa jingine kwani alikua hampendi MARRY..
MARRY alienda kwaakina ESTER ili kumjulisha juu ya safari yake..alipofika kule alimkuta ESTER na baba ake wanajadili kuhusu ESTER kwenda DAR kufungua SALOON YA KIKE...baba ake alitaka mwanae akakae kwa baba yake mdogo ambae anaishi MBAGALA jijini DAR...lakin baada ya MARIA kuwaeleza kua nae anaenda kukaa huko dar kwenye nyumba ya marehemu mama ake ndipo wakaona ni bora wakakae wote huko kwani walikua ni marafiki toka utotoni mpaka sasa wote wamefeli kidato cha nne..
Walikubaliana na maandalizi yalipokamilika wakasafirishwa wao na vitu vyao hadi DAR ambapo walifika salama....kwakua nyumba ile hakuishi mtu kwa mda mrefu hivyo walianza kufanya usafi huku vyombo vyao vikiwa nje na walomaliza wakaingiza ndani na kuvipanga katika mpangilio mzuri ambao unadhihirisha kua usafi na ustaarabu unachukua nafasi yake kwa wasichana wale ambao kiuhalisia walikua wazuri tena sio ule uzuri wa make up..ulikua ni uzuri wa asili kwani MARRY alikua ni mweusi kiasi yan ule weusi wa kung'aa,umbo lake zuri na macho madogo ya kijivu na ESTER alikua na ngoz ya maji ya kunde,umbo modo lakin lile lenye mvuto..
Wakiwa wanamalizia kutandika kitanda na sofa mlango uligongwa kistaarabu kidogo....
#ITAENDELEA panapo majaaliwa
Posted via Blogaway