Kati ya vitu ambavyo husaidia kuongeza thamani ya msanii katika
macho ya mashabiki ni pamoja na watu kuona akipata dili kubwa
na kulipwa pesa nyingi katika shows.Lakini kumekuwepo baadhi
ya wasanii ambao wakati mwingine hutengeneza mazingira ya
uongo hasa kupitia mitandao ya kijamii, na wengine hata kufanya
na Interviews ili tu kufanya watu waamini kuwa thamani yao pia
iko juu.
Mzungu Kichaa yuko tofauti kidogo katika hilo, sababu haoni
sababu ya msanii kudanganya kwa kitu ambacho sio kweli.
Msanii huyo wa Denmark aliyeishi Tanzania kwa miaka mingi
alizunguzungumzia swala hilo katika kipindi cha Sporah.
“Mimi siwezi kwenda kwenye vyombo vya habari na kusema ooh
nimetengeneza milioni 100 kwenye show halafu media zote
ziseme ‘oooh wow’…kama alivyofanya Alikiba kipindi fulani”
Alisema Mzungu Kichaa. “Alisema alikuwa anataka kwenda
kufanya show Ujerumani, na alikuja kusema ameahirisha kwenda,
tena aliahirisha siku moja kabla, na kusema kuwa angelipwa
shilingi milioni 100…Kwahiyo akadai kwamba alikuwa anapewa
hiyo hela lakini mikataba haikwenda kama ilivyotakiwa so
aliahirisha show siku moja kabla, na kama mwanamuziki mimi
najua jinsi mambo ambavyo hua yanakuwa, siamini watu
waliokuwa tayari kumlipa kiasi cha pesa kama hicho…na kwa wao
kutafuta media publicity kupretend we are getting big money to
perform nadhani hilo ni kosa.” Alimaliza
Posted via Blogaway
No comments:
Post a Comment