April 27 kulitokea vifo vya watoto 3 ambao walikua na
birthday party nyumbani lakini baada ya kukamilika kwa
taratibu za party ya nyumbani waliamua kuimalizia party
hiyo hotel ya Landmark,walipofika walienda kuogelea
kwenye swimming pool ya watoto lakini baadae watoto hao
walitoka kwenye pool ile ya watoto wakaingia kwenye pool
ya wakubwa na kwa bahati mbaya waliingia sehemu yenye
kina kirefu.
Watoto wenzao walipoona wenzao wanazama walianza
kuwavuta kuwatoa nje lakini hali zao tayari zilikua
mbaya,mmoja wapo hali yake ilikua kidogo afadhari lakini
kwa bahati mbaya nayeye alifia hospital wakati akipatiwa
matibabu katika hospitali ya Masana na kufanya Idadi ya
watoto waliofariki kuwa 3 majina yao ni Janet Zacharia,Eva
na Ndimbuni.
Kamanda Kova amesema>>’Kusema kweli sio mara ya
kwanza kutokea,mara nyingi vifo vya watoto vinatokana na
uangalifu au uzembe kutoka kwa wale wanaotakiwa
kuwaangalia hao watoto wao,hizi hotel zote zenye
swimming pool lile eneo la kuogelewa basi wasiruhusiwe
watoto wadogo kuogelea au kuwe na mtu ambaye anajua
kuogelea au kuokoa ambaye yupo pale’
‘Unajua watoto wana tabia ya kuigana mmoja akiingia
akiogelea pengine anafahamu kidogo wengine wote
wanafata mkumbo wanaona wanaweza,sisi kama jeshi la
Polisi tumeamua hili kosa la uzembe kusababaisha kifo
kisheria mtu anaweza kushtakiwa kwa kuzembea kwa
kutochukua tahadhari mpaka watoto kama wale ambao
hawana hatia uwezo wao mdogo wa kufikiri au kuijiokoa’
‘Tunafatilia kwa umakini lakini jukumu la kufatilia maisha
ya watoto ni la wazazi mia kwa mia wasipofanya hivi
wakiwa hawapo makini matokeo yake ni haya watoto 3
wamefariki,tunaendelea na uchunguzi na baadae tutatoa
taarifa kamili’.
Posted via Blogaway
No comments:
Post a Comment