Saturday, October 4, 2014

KESI YA MWANAFUNZI ALIYELAWITIWA YAFUTWA

Kesi ya mwanafunzi wa darasa la tatu
(jina linahifadhiwa) katika Shule ya
Msingi Ukombozi iliyofunguliwa
katika Kituo cha Polisi cha Urafiki,
jijini Dar es Salaam baada ya kudaiwa
kulawitiwa imefutwa.
Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa
Septemba 15, mwaka huu kituoni
hapo, ikimkabili mtuhumiwa
aliyetajwa kwa jina moja la Enock,
imefutwa jana na mtu huyo kuachiwa
huru kwa madai kuwa, imekosa
ushahidi.
Mama wa mtoto huyo (jina
linahifadhiwa), aliliambia gazeti hili
kuwa, mpelelezi wa kesi hiyo
aliyemtaja kwa jina moja la Suzana
aliiambia familia hiyo kuwa, baada ya
jalada la kesi kupelekwa kwa
mwanasheria na kulipitia, alikosa
ushahidi wa kulipeleka shauri hilo
mahakamani.
Alisema baada ya kuripoti tukio hilo
kituoni hapo alipewa RB/
Urafiki/7627/2014.
Aidha, mama huyo alisema mjomba
wa mtoto alipofuatilia kesi hiyo jana
kituoni hapo alirudi na majibu kuwa
imefutwa.
Alisema kuwa baada ya kukutana na
mpelelezi wa kesi hiyo, alimweleza
kuwa jalada la kesi limerudi kutoka
kwa mwanasheria na mtuhumiwa
anaachiwa huru kutokana na
kukosekana ushahidi.
Alisema baada ya maelezo ya
mpelelezi, aliomba kuonana na Mkuu
wa Kituo hicho, ambaye naye
alimweleza kuwa, majibu ya daktari
yalionyesha hajalawitiwa.
Pia alisema mkuu huyo wa kituo
alimweleza kuwa alichokieleza mtoto
kuhusu mazingira ya nyumbani kwa
mtuhumiwa yalikutwa tofauti.
Siku ya tukio mtuhumiwa huyo
alikamatwa baada ya mama
kuambatana mtoto wake siku ambayo
kijana huyo alikuwa na miadi ya
kukutana na mwanafunzi huyo.
Kabla ya kukamatwa kwake, kijana
huyo ilidaiwa alishamfanyia vitendo
hivyo mtoto huyo zaidi ya mara moja
na alikuwa akimpa fedha kati ya Sh.
2000 na Sh. 7000 lakini siku ya
kukamatwa alimpa Sh. 200.
Awali, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,
Biamina Swai, aliliambia gazeti hili
kuwa, kwa mwaka huu jumla ya
matukio manne ya watoto kufanyiwa
vitendo hivyo yalitokea lakini hilo
moja ndilo mtuhumiwa wake
alikamatwa baada ya kushirikiana na
mzazi wake.
Alisema matukio mengine baada ya
wazazi kupewa taarifa za ulawiti wa
watoto wao, pindi waendapo mitaani
huvujisha siri na kusababisha
wahusika kukimbia.

No comments:

Post a Comment