Saturday, October 4, 2014

WANAUME 400,0

Serikali imesema jumla ya wanaume
400,000 kutoka mikoa minne nchini,
wamefanyiwa tohara katika kampeni
iliyomalizika hivi karibuni.
Katika hotuba ya Waziri wa Afya na
Ustawi wa jamii, Dk, Seif Tashid,
iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, John Michael, wakati wa
ufungaji wa kampeni hiyo jijini Dar es
Salaam jana, alisema mikoa
iliyohusika na kampeni hiyo ni Iringa,
Njombe na Tabora.
Zoezi la kuwafanyia tohara wanaume
lililofahamika kama `tohara ya
kitabibu ya wanaume’ (VMMC)
iliendeshwa kwa ushirikiano kati ya
Serikali ya Tanzania, Marekani na
Shirika la Jhpiego.
Alisema zoezi hilo limesaidia
kupunguza kasi ya maambukizi ya
virusi vinavyosababisha Ukimwi
(VVU) nchini, kitu kinachoonyesha
lengo la kufikia maambukizi ya
asilimia 0.16 hadi mwaka 2018
linaweza kufikiwa.
Baada ya kuonekana kwa mafanikio
hayo, mikoa mingine 12 ambayo
wanaume wake wapo nyuma katika
kufanyiwa tohara imeteuliwa
kuendelea na zoezi hilo.
Kiasi cha Dola za Marekani Milioni 34
zimetengwa kwa ajili ya kuendesha
kampeni hiyo.
Dk. Rashid alisema lengo ni kuwafikia
watu milioni 2.1 walio na umri kati ya
miaka 10 hadi 34 kufikia mwaka 2017.
Awali, Naibu Mkurugenzi wa Shirika
la Misaada la Marekani nchini (USAID)
, Timoth Donny, alisema katika tafiti
mbalimbali zinaonyesha kwamba
wanaume waliofanyiwa tohara
wanaondokana na hatari ya
kuambukizwa VVU kwa silimia 60,
hivyo kuna wajibu wa kuhakikisha
elimu inatolewa sehemu zote nchini.
Alisema nchi yake ipo tayari kusaidia
katika kupambana na hali hiyo katika
nyanja ya kujengea uwezo wa
mafunzo na vitendea kazi kwa watoaji
huduma.
Naibu Rais wa Shirika la Jhpiego,
Alain Damiba, pamoja na kuishukuru
serikali kwa kutoa msaada mkubwa
katika kutekeleza mkakati huo, shirika
lake kwa kushirikiana na washirika
mbalimbali litaendelea kufanya kazi
kwa ajili ya kuboresha afya za
wananchi na kuongeza kasi ya
maendeleo.

No comments:

Post a Comment