Tanzania imeporomoka tena kwenye
viwango vya soka vinavyotolewa kila
mwezi na Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa), baada ya kuanguka
kwa nafasi tano katika viwango
vilivyotolewa jana.
Tanzania, ambayo ilifungwa 2-0 na
Burundi katika mechi ya kimataifa ya
kirafiki iliyopita, sasa inakamata
nafasi ya 115 duniani na 33 barani
Afrika ikiwa nyuma ya Uganda
wanaoongoza Afrika Mashariki
wakiwa nafasi ya 79 duniani na 19
Afrika, Rwanda walioko nafasi ya 93
duniani na 25 Afrika na Kenya
walioporomoka kwa nafasi saba
wakiwa nafasi ya 30 Afrika na 111
duniani.
Aligeria waliopanda kwa nafasi nne,
wanaongoza barani Afrika wakiwa
nafasi ya 20 duniani wakifuatwa na
Ivory Coast walioshuka kwa nafasi
tatu baada ya kukubali kichapo cha
mabao 4-1 kutoka kwa Cameroon
waliopanda kwa nafasi 12 na
kukamata nafasi ya nane Afrika na 42
duniani.
Nafasi ya tatu barani Afrika inakaliwa
na Tunisia (31) wakipanda kwa nafasi
11 wakifuatwa na Ghana (33), Senegal
(36), Nigeria (37) na Cape Verde (41).
Guinea waliopanda kwa nafasi 16
wanakamata nafasi ya tisa barani
Afrika na 48 duniani huku Burkina
Faso waliopanda kwa nafasi 10
wakifunga pazia la 10 bora barani
Afrika wakifungana na Guinea katika
nafasi ya 48 duniani.
Uganda pia ni wa kwanza katika
Ukanda wa Cecafa wa Afrika Mashariki
na Kati wakifuatwa na Rwanda,
Kenya, Tanzania, Burundi, Ethiopia
(39, 132), Sudan (40, 133), Shelisheli
(47, 172), Sudan Kusini (50, 185),
Eritrea (52, 202), Somalia (53, 204)
huku Djibouti wakifunga mlango
Cecafa na Afrika wakiwa 54 Afrika na
205 duniani.
Mabingwa wa dunia, Ujerumani
wanaongoza 10 bora ulimwenguni
wakifuatwa na Argentina, Colombia
waliopanda kwa nafasi moja
wakiwashusha Uholanzi, Ubelgiji,
Brazil, Uruguay, Hispania, Ufaransa
na Uswis.
Thursday, September 25, 2014
TANZANIA YASHUKA VIWANGO FIFA
Labels:
michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment