Thursday, August 14, 2014

Cheka ila usiharibu mbavu

Mhindi alijibu mtihani wa Kiswahili kama ivi:

(1) Mfa maji ?....ipatie life jacket, lambda taokoka.

(2) Mwenda pole?....... Tachelewa fika.

(3) Usipoziba ufa ?........... Mizi tachungulia  dani.

(4) Usilolijua ?........ Uliza google.

(5) Mbio za utelezini ?..itaChafua guo yako.

(6) Ukipenda boga ?...Ngoja mezi ya ramzani tapata rahisi.

(7) Ukiona vinaelea ?.iko nyepesi sana hiyo.

(8) Maji yakimwagika ?...... Mambie dada tapiga deki.

(9) Chelewa chelewa ?... Takosa mapesa veve.

(10) Kila ndege huruka ?... Airport

(11) Bandu bandu ?...du gu Yale pateli na sa sa ipo Bombey.

(12) Mtaka cha Mvunguni ?..sharti inue tanda

(13) Simba mwenda kimya?....Kama sio gonjwa basi haina njaa.

(14) Aisifuye mvua ?.......... Najua iko Mkulima hiyo

(15) Barabara ndefu ?........ Ongeza mwendo au tachelewa fika.

(16) Mlanawe hafi nawe ila?.... Takimbia

(17) Asie sikia la mkuu ? ........ Tapeleka jela

(18) Hasira za mkizi ? ..............Tatafuna veve

(19) Mchamba wima ?........ Karibu ya Hurumzi

(20) Akumurikae mchana ?....Kipofu hiyo

(21) Mficha maradhi ?........ Taenda Loliondo

(22) Mkataa wingi ? ..........Taenda Chadema

(23) Bendera ?................ Kama sio ya ODM, ya TNA

(24) Baniani mbaya ?....... Peleka Bombay Lakini sio kweli, naonea tu

(25) Akili nyingi ?.......... Tapasi mtihani yotee

(26) Penye kuku wengi ? ........ Chinja bili tatu ivi, hapana mtu najua.

No comments:

Post a Comment