Wednesday, August 13, 2014

JE WAJUA KUA RIHANNA ANATAKA M KUNUNUA CLUB KUBWA UINGEREZA? CHECK HAPA

Moja ya watu maarufu waliokumbwa
na joto kubwa la soka wakati wa
michuano ya kombe la dunia, alikuwa
ni mwanamuziki Rihanna.
Alikuwa akituma tweets karibia
kwenye michezo yote na mwishoni
alienda kuhudhuria fainali ya
michuano hiyo iliyopigwa kwenye
dimba la Maracana kati ya Ujerumani
dhidi ya Argentina.
Siku kadhaa nyuma gazeti la Daily
Mail la Uingereza liliripoti kwamba
staa huyo alikuwa anajiandaa
kununua hisa kwenye moja ya vilabu
vikubwa nchini Uingereza, lakini
hawakutaja jina la timu.
Lakini leo hii Jumanne, gazeti moja
huko Catalunya liitwalo El Mundo
Deportivo limethibitisha kwamba
Rihanna anataka kununua hisa nyingi
kwenye klabu ya Liverpool.
Rihanna amewahi kuripotiwa kwamba
anaishabikia klabu ya Liverpool,
jambo ambalo inawezekana El Mundo
Deportivo wamemhusisha na ununuzi
wa klabu hiyo ya Anfield.
Liverpool kwa sasa inamilikiwa na
mmiliki wa makampuni ya American
Fenway Sports Group John W. Henry.

No comments:

Post a Comment