Saturday, October 4, 2014

PHIL AAHIDI MABADILIKO YA SIMBA

Simba itakayoingia Uwanja wa Taifa
kucheza mechi yake ya tatu ya ligi
kuu ya Bara dhidi ya Stend United leo
baada ya sare mbili mfululizo itakuwa
kama mpya, kocha Patrick Phiri
amesema.
Akizungumza na gazeti hili jana, Phiri
alisema katika mchezo wa leo
atafanya mabadiliko kwenye kikosi
chake ili kuweka uwiano kati ya ulinzi
na mashambulizi kwenye kikosi.
Phiri alisema "Tumechoshwa na
matokeo ya sare" na kwamba
amefanya marekebisho kwenye kikosi.
"Kama utakuwepo uwanjani utaona.
Lengo ni kuiimarisha timu ili kuleta
ushindi."
Kocha huyo Mzambia alisema ushindi
kwenye mchezo wa leo utawarudisha
wachezaji wake 'kwenye njia' baada
ya sare za nyumbani za 2-2 dhidi ya
Coastal Union na 1-1 dhidi ya Polisi
Morogoro.
"Baada ya mchezo dhidi ya Stand
United tutakutana na wapinzani wetu
(Yanga)... nimewaambia wachezaji
tunahitaji ushindi kabla hatujakutana
nao."
Simba ambayo inapewa nafasi kubwa
ya kufanya vizuri msimu baada ya
kumridisha Phiri aliyeipa ubingwa bila
kupoteza mechi mwaka 2010, ipo
pointi nne nyuma ya timu mbili
viongozi mabingwa watetezi Azam na
Mtibwa Sugar.
Aidha, aliwataka mashabiki wa timu
hiyo kutokata tamaa na timu yao
kwani Simba ni timu nzuri na makosa
ya yanayoonekana yanarekebishika na
kuomba kupewa muda kwa wachezaji
wake.

No comments:

Post a Comment