Friday, October 3, 2014

TAMBWE AMTANGAZIA VITA KAVUMBAGU

Mfunguji bora wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu
uliopita, Amissi Tambwe amesema
ataanza 'kumshika' kinara wa mabao
kwa sasa Didier Kavumbagu kesho
wakati Simba itakapoivaa Stand
United kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.
Kavumbagu, mshambuliaji wa Azam
FC na timu ya taifa ya Burundi
'Entamba Murugamba', anaongoza
safu ya wafumani nyavu akiwa
amefunga mabao manne katika mechi
mbili za mwanzo ambazo mabingwa
hao watetezi walishinda 3-1 dhidi ya
Polisi Morogoro na 2-0 dhidi ya Ruvu
Shooting.
Hata hivyo, Tambwe katika mahojiano
na chanzo chetu  jijini Dar es Salaam jana
alisema zawadi ya mfungaji bora
itatua tena kwake na ataanza
kufukuzana na Kavumbagu katika
mechi ya kesho.
"Ninaona ametangulia tu, Simba kwa
sasa imeimarika, ninaamini tutaanza
kushinda kwa magoli mengi kuanzia
mechi inayokuja," alisema.
"Kikosi chetu kimeanza vibaya
kutokana na matatizo kidogo ambayo
tuliyazungumza kwenye kikao na
uongozi jana (juzi). Kazi yangu ni
kufunga, nitafunga zaidi yake,"
alisema zaidi Tambwe.
Raia huyo wa Burundi anayesifika kwa
kufumania nyavu, alijiunga na Simba
Agosti mwaka jana akitoka kuipa
ubingwa wa Kombe la Kagame klabu
ya Vital'O ya kwao, Burundi.

No comments:

Post a Comment