Friday, October 3, 2014

WATANZANIA WANG'ARA KATIKA CHAGUO LA VIONGOZI WACHUMI WA KESHO AFRI

Watanzania watano wamechaguliwa
kuingia katika orodha ya viongozi
wachumi wa kesho 100 akiwemo
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Mohammed Enterprises Tanzania
Limited (MetL), Mohammed Dewji.
Dewji ambaye pia ni Mbunge wa
Singida Mjini, alishika nafasi ya pili
kupitia utafiti wa kila mwaka
uliofanywa na Taasisi ya Choiseul ya
Ufaransa inayojishughulisha na
uchambuzi wa masuala ya kisiasa,
kiuchumi na utamaduni kimataifa.
Watanzania waliongia kwenye orodha
hiyo ma kampuni zao katika mabano
ni Genevieve Sangudi (Carley Group),
Elsie Kanza (Mkuu wa World
Economic Forum-Afrika), Patrick
Ngowi (Helvetic Group) na Denis
Dilllip ambaye ni Mwenyekiti wa
Canaco Tanzania.
Viongozi hao wamechaguliwa na
taasisi hiyo kwa kuangalia michango
ambayo wametoa katika mataifa yao
na Bara la Afrika kwa ujumla
yakiwamo kutoa ajira, uwekezaji wa
ndani na nje na uinuaji wa uchumi
kupitia biashara wanazofanya.
Katika orodha hiyo nafasi ya kwanza
imeshikwa na Igho Sanomi (Nigeria),
Mohamed Dewji ya pili, , Hisham El
Khazindar wa Misri (3), Isabel Dos
Santos wa Angola (4), Tidjane Deme
wa Senegal (5), Nomkhita Nqweni wa
Afrika Kusini (6), Mehdi Tazi wa
Morocco (7), Marlon Chigwende wa
Zimbabwe (8) huku nafasi tisa ikienda
kwa Ashish Thakkar wa Uganda
wakati ya kumi imechukuliwa na
Janine Diagouwodie wa (Ivory Coast)

No comments:

Post a Comment