Tuesday, April 22, 2014

AL-SHABAAB WATOA TISHIA LA KUFA MTU DHIDI YA KENYA

Tishio la kigaidi lina kodolea macho taifa la Kenya baada
ya kundi la kigaidi lililo na makao yake makuu nchini
Somalia kuachia video nyingine kwenye mtandao wa Al-
Kataib wakitishia kutekeleza mashambulizi nchini Kenya
wakati wowote.
kwenye kanda hiyo msemaji wa alshabaab aliye jifunika
uso anasema kwamba hawaoni lolote litakalo wa zuia
kuingia Kenya hasa baada ya kufanikiwa kutekeleza mauaji
katika jengo la west Gate. mwaka uliopita>>’tumekuwa
tukisema tutafika Kenya lakini hivi tayari tushafika si eti
westgate ndio tosha bado kuna mamia na mamia ya watu
wanaongojewa mahala kama hiyo insha Allah’alisema
msemaji huyo.
Huku wakiimbia tutawalipua hadi tuwamalize wanamgambo
hao wamesema kwamba wameamua kuungana na
wasomali kutetea dini ya Allah,Wadadisi wa maswala ya
kiusalama wanahoji kwamba huenda hawa ni baadhi ya
vijana kutoka kwa mataifa ya Afrika mashariki walipewa
mafunzo ya itikadi kali na baadaye kupelekwa somalia
kujiunga na Alshabaab kutokana na wanavyozungumza
lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kwenye video hiyo.
Ispekta mkuu wa polisi nchini Kenya bwana David kimaiyo
amesema uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha
video hiyo na taarifa kamili kutolewa punde tu watakapo
pata habari zaidi kuhusiana na video hiyo.

EE MUNGU TUJALIE AMANI WAJA WAKO


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment