Tuesday, April 1, 2014

EMINEM ATAKA KUWEKA BIFU NA KANYE WEST NA LIL WYNE....Princenordy

Eminem ambae ni msanii wa hiphop wa
miaka mingi amezungumzia kitu kipya
kuhusiana na wimbo wake wa ‘Talking 2
Myself’ kutoka kwenye album yake ya
‘Recovery’ iliyotoka June 2010
Anasema ni wakati ambao alijikuta kuwa ni
hater tu na kwamba alitaka kuwazungumzia
vibaya Kanye West na Lil Wayne ambao
walikuwa mbali kimuziki time hiyo.
Namkariri akisema ‘nilikichukia kitu chochote
ambacho kilikua kikipendwa (kipo hot) kwa
muda ule au mtu yeyote aliekua akifanya
vizuri kwa muda ule, baadae nilijiskia vibaya
mimi mwenyewe na muziki niliokua
nikiutengeneza kipindi hicho, nilijihisi kuanza
kubadilika kuwa hater yani nikawa
nachukiachukia tu watu na vitu ovyo’
Lil Wayne na Kanye West
Kingine cha mwisho alichosema Eminem ni
kwamba angeweza kujiua kwa hali hiyo
aliyokua nayo kama ya kuchanganyikiwa wakati
huo, sio tu kuwachukia Kanyewest na Wayne
bali kuna mengine mengi pia aliyawaza.


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment