Tuesday, April 1, 2014

MAMBO MATATU KUHUSU MTOTO ALIEBAKI NA RISASI KICHWAN....

Ni mtoto Satrin Osinya ambae mama yake
mzazi aliuwawa kwenye shambulio lililofanywa
kanisani huko Mombasa Kenya ambapo watu
waliokua na silaha walishambulia kwenye
ibada ikabidi mama amkinge mtoto,
ikisemekana risasi iliyofyetuliwa ikamuua
mama na kupenyeza mpaka ikagota kichwani
kwa mtoto aliebaki hai.
Satrin mwenye umri wa mwaka mmoja na
miezi sita alibaki na hiyo risasi kichwani toka
shambulio hilo lilipotokea zaidi ya wiki moja
iliyopita.
1. Madaktari katika hospitali ya Kenyatta
Nairobi Kenya wamefanikiwa kuitoa risasi hiyo
April 1 2014 baada ya kazi ya dakika 180
ambapo sasa mtoto huyu hayupo tena kwenye
hatari ya kupoteza maisha.
2. Kikundi cha Madaktari 12 bingwa wa
kichwa ndio kimeifanya hii kazi.
3. Madaktari wanasema mtoto huyu ameanza
kuongea, kucheza na hata kusogea tofauti na
mwanzo.


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment