Sunday, April 20, 2014

WAUMINI NCHINI KENYA KUSAFISHA BARABARA KWA SABUNI...

Kupitia vyanzo vyetu nchini Kenya riporter wetu anaripoti
kwamba wakazi wa jiji la Eldoret wamemfanya kila alieiona
hii kuvutiwa na pengine kujua imekuaje wakafanya hivi kwa
mara ya kwanza baada ya kujitosa na kupiga deki barabara
ya lami ya Oginga Odinga jijini Eldoret kaunti ya Uasin
Gishu nchini Kenya.
Unaambiwa wameamua kufanya hivi ikiwa ni maandalizi ya
kumlaki nabii Daktari Awuor kwa ajili ya maombi ya leo na
siku ya Jumatatu kuadhimisha pasaka na kumshukuru
jehova kwa kuwasaidia jiji la Eldoret kufanyika uchaguzi wa
amani mwaka 2013
Hata hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii maoni
yalikotolewa na Wakenya kuhusu hii ishu, maoni mengi
yameonekana kupinga kitendo cha waumini hao wa kanisa
la Jesus is lord kwa kumpa Daktari Awuor heshima kupita
kiasi.
Mkurugenzi mkuu wa Kass media inayo miliki Radio ya
kass fm inayotangaza kwa lugha ya kikalenjin
inayozungumzwa na wakazi wa jiji la Eldoret Julius lamaon,
amesema ‘watu wetu waache kupotoka, jiji letu
limebadilishwa na kuwa jiji la vituko…… Gavana hatakiwi
kuhudhuria mkutano huu’


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment