Friday, April 4, 2014

NEY WA MITEGO AELEZA SABABU YA KUTAKA KUMUOA SIWEMA....

MWANAMUZIKI Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’
amesema yupo kwenye mikakati ya kufunga pingu za
maisha na mpenzi wake anayejulikana kwa jina la
Siwema baada ya kumtundika mimba.
Nay akiwa na mpenzi wake Siwema.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Nay
alisema anajivunia kukaribia kuitwa baba na kizuri ni
kwamba msichana aliyempa mimba alikuwa na ndoto za
kumuita mke wake hivyo ndoa itafungwa kabla ya mtoto
kuzaliwa.
“Kikubwa naomba Mungu mipango yangu iende kama
nilivyopanga kwa sababu nataka kabla mtoto hajazaliwa
tuwe ni wanandoa tunaotambulika kwa Mungu kwa
kufunga pingu za maisha,” alisema Nay.
Akizungumzia kubebeshwa mimba na msanii huyo,
Siwema aliliambia Ijumaa: “Najisikia furaha sana
kumbebea mimba Nay, tumetoka mbali naamini ndoto
yetu ya kuoana itatimia siku si nyingi.”
at Editor  8:43 PM


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment