Saturday, April 19, 2014

STORY MPYA...

Story:BATA MREFU
writter: ALNORD SPORTIEVE

""We ALNORD....anodiiii,,,,,,we mtoto wa mzee mgumba.....hunisikii au ndo kiburi???"

Ilikua ni sauti ya ukali kidogo na utani ndani yake aliokua akiitoa Se Mlowe ambae ni mke wa mzee SPORTIEVE ANYELWISE MGUMBA na mama wa mtoto mmoja(alnord) ambao walikua wakiishi katika kijiji cha MFUMBI kilichopo CHIMALA-MBEYA...aliekua akimuita mwanae mpendwa aliekua amekuja kuchukuliwa na KAKA ake (RAJAB ABDALLAH CHUMA)ambae ni mtoto wa baba ake mkubwa(ABDALLAH  CHUMA) alieshiriki mama mmoja ila baba tofauti na baba ake mzee SPORTIEVE MGUMBA.... ili aende nae mjini DAR-ES-SALAAM kumsaidia kusimamia botique(duka la nguo) ambalo ni la baba ake..

Ilibidi aitwe Alnord kwenda huko baada ya wafanyakazi wengi waliowaajili kutokua waaminifu kwani walikua wakiiba pesa ikiwa ni pamoja na nguo na kukimbia....hivo wakaona kumleta ndugu yao huyo inaweza ikaleta ahueni...maana RAJAB aliezoeleka kwa jina la CHUMA ambao ndio ubini wake alikua bize na masomo na mara nyingi kwenda kwenda kufunga mzigo ambao mara nyingi huenda kufungia CHINA..

Basi ALNORD alimaliza kujiandaa akiwa kavalia nguo zake alizonunuliwa katika kusherehekea kuvuka mwaka mpya ali maarufu kama NEW YEAR na kwenda nje ambapo alikua akisubiriwa na kaka yake huyo...

Alifika pale na kupewa baraka na wazazi wake huku wakimsihi kua mwaminifu katika biashara ya baba yake mkubwa na pia kuwa mnyenyekevu na mtiifu pindi awapo nyumbani kwa baba yake mkubwa....mama ake alimsisitizia sana kuhusu swala la kujifanya mjinga kwa kila atakachoambiwa na pia kuepuka kujiingiza katika mapenzi kwani walikua wakisikia kua dar es salaam kulikua na vishawishi vingi ambavyo vingepelekea kupata maambukizo ya UKIMWI...walimsihi sana maana hawakupenda mwanao wa pekee ambao walimpenda kupita maelezo kwani ndiye waliebarikiwa na MUNGU...

Alnord aliahidi kuyazingatia hayo kisha wakaagana na huku wazazi wake wakimpa mikono ya kheri kuashiria kua wanamtakia safari njema..

#ITAENDELEA panapo majaaliwa
Support yako ni muhimu sana


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment