Thursday, April 17, 2014

IFUATAYO NI TAARIFA FUPI YA MPIGA GUITAR WA SKYLIGHT BAND ambae kwa sasa amefariki dunia....

Aliyekua mpiga Bass Guitar wa Skylight Band amefariki
dunia usiku wa kuamkia leo April 17,Marehemu Ayubu
songolo ama Chili Chala ambaye alizoeleka kwa jina hilo
amefariki ghafla ambapo taarifa inasema alianguka akiwa
nyumbani kwake.
Marehemu Alikimbizwa hospitali akiwa amepooza mwili na
ameacha Mke na watoto wawili,miongoni mwa bendi
alizowahi kuzifanyia kazi ni bendi ya Akudo Impact,Fm
Academia na mwaka jana alijiunga na Skylight
band,mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake
Mwanyamala B karibu na msikiti wa Hidaya.
Kuhusu Onyesho ambalo huwa linafanywa kila Alhamisi
Escape One na Skylight Band,wametangaza kuahirisha
kutokana na msiba huu. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA....JIANA LA BWANA LIHIMIDIWE(INA LILLAH WA INA LILLAH RAJUN)


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment