Sunday, April 6, 2014

PASTOR ANASWA AKIFANYA UFUSKA KWENYE DANGURO.....

OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers
inaendelea! Wiki hii ilifanya kazi nyingine nzito, kumnasa
Pastor John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la
Maximum Deliverance lililopo Masaki, Dar ambaye alinaswa
akichezewa utupu na wanawake watatu ambao ni kama
waumini wake kwa sababu wote ni Wakristo.
Pasta John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la
Maximum Deliverance lililopo Masaki, Dar baada ya
kunaswa na wanawake watatu wakimchezea utupu.
OFM YATONYWA UCHAFU WA PASTOR Ilikuwa Jumanne ya
Aprili Mosi, 2014, saa 4:14 asubuhi, chanzo cha habari
kilipiga simu chumba cha habari cha Global na kuwataka
makachero wa OFM ambapo alipounganishwa nao alisema:
“Jamani kama kweli hapo ni OFM nina malalamiko. Mimi
nimeshtukia mchezo mchafu unaotaka kufanywa na pastor
(mchungaji) mmoja anaitwa Rubanguka.
Pasta John Paul Simon Rubanguka akijaribu kujitetea.
“Huyu pastor amempa dili dada mmoja kumtafutia
wasichana wazuri watatu na kuwapeleka kwenye nyumba
moja hivi kisha wawe wanamchezea utupu wake huku wao
wakiwa kama walivyozaliwa, ndiyo furaha yake ilipo.
Wasichana wameshapatikana.”
Makamanda wa Polisi wakimbananisha na kumtuliza
Pasta huyo ili apunguze munkari.
MSHIKO WA NGUVU NA SAFARI JUU Mtoa habari huyo
aliendelea kudai kuwa, pastor huyo alisema wasichana
watakaokuwa wakichezea utupu atawafanyia usaili wa kwenda
kuwauza kwenye kasino moja iliyopo Uarabuni ambayo yeye
ni wakala wa kuwapelekea malaya huko.
Pastor
akiwa na mmoja wa wanawake waliofumaniwa naye.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, pastor huyo aliwaahidi
wanawake hao kitita cha shilingi 300,000 kila mmoja kwa
wale watakaofaulu kumchezea vizuri, sanjari na kuwakatia
hati za kusafiria ‘passport’.
Makamanda wa OFM wakimtuliza Pasta.
OFM YAWEKA MTEGO Baada ya kupata ishu nzima, OFM
ilifanya ukachero na kugundua mahali ambapo tukio hilo
lilipangwa kufanyika, ni kwenye danguro moja lililopo
Kinondoni jijini Dar.
Wanawake walionaswa katika tukio hilo wakivaa viwalo
vyao.
OFM ilifika kwenye nyumba hiyo na kufanya ushushushu
wake ambapo walifanikiwa kuweka mitambo yao sambamba
na kulishirikisha jeshi la polisi kwa ajili ya kumnasa
mtumishi huyo wa Mungu akifanya vitendo hivyo.
Saa 8:11 mchana, OFM wakiwa wamejibanza eneo hilo
waliwashuhudia warembo watatu, weupe wakielekea kwenye
nyumba ambayo mtoa habari wetu aliielekeza.
Kitambulisho cha Pasta.
PASTOR AWASILI KWA MBWEMBWE Saa 11:23 jioni, OFM
wakiwa hawajaanza hata kujisikia kuchoka, walimwona pastor
huyo akiwasili kwa mbwembwe akiwa ndani ya gari dogo na
kugeuza kwa staili ya kupiga ‘norinda’ kisha akashuka.
Mkononi alishika maji makubwa. Alipokelewa na mmoja wa
wanawake hao.
Bango lililopo Kinondoni Mkwajuni, Dar likieleza lilipo
kanisa la Pasta huyo.
MCHEZO WAANZA Saa 11:40 jioni, makachero wa OFM
walifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa, tayari mchezo
ulishaanza ambapo waliwataarifu polisi na kuungana nao
kwenda kuvamia nyumba hiyo.
Msafara wa OFM na polisi hao ulifika nje ya chumba
kilichokuwa kikidaiwa kufanyika uchafu huo. Sauti ya muziki
na wanawake waliokuwa kama wapo kwenye darasa la siri
zilisikika.
Polisi waligonga mlango na kujitambulisha kisha wakaomba
wafunguliwe mlango haraka ndani ya sekunde chache.
PASTOR APATA MCHECHETO Pasta John na wanawake hao
walitii amri kwa kufungua mlango ambapo mchungaji huyo
alikumbwa na mchecheto na kutaka kurukia juu ya dari lakini
polisi walimtafadhalisha kutulia pamoja na wanawake hao
kama walivyo.
OFM ikiwa chumbani humo iliwashuhudia wanawake hao
wakiwa watupu mbele ya pastor huyo ambapo walikuwa
wakimnengulia viuno.
Baada ya kupewa kibano, warembo hao walimwanika pastor
huyo kwamba ndiye aliyewatuma wamchezee wakiwa watupu
ili awalipe shilingi laki tatu kila mmoja, pia kuwapeleka
Uarabuni kwenye kasino.
UTETEZI WA PASTOR Kwa upande wake, Pastor John alijitetea
kuwa anaomba asamehewe kwa gharama zozote ili taarifa
hizo zisifike popote kwani ishu hiyo ilikuwa si amri yake bali
shetani alimpitia.
“Jamani naomba tumalize humuhumu ndani, mnajua mimi
ni Pastor wa Kanisa la Maximum Deliverance, sasa ukweli ni
kwamba waumini wangu hawatanielewa, chondechonde
ilindieni kazi yangu jamani,” alijitetea.
Mpaka OFM inaondoka eneo la tukio, pastor huyo na
wanawake ‘wake’ walikuwa kwenye harakati za kupelekwa
mbele ya vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zinazostahili.
KUTOKA MEZANI KWA MHARIRI Siku zote kazi ya OFM ni
kuwajibikia matendo maovu na si kuwaonea watu  kwa lengo
la kuwachafua. OFM inapopata habari huichunguza ukweli
wake kwanza kabla ya kuchukua hatua ya kuifanyia kazi moja
kwa moja, yaani kufika kwenye eneo la tukio.


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment