Friday, April 4, 2014

WATU WALIOFUNIKWA NA KIFUSI LEO HUKO BUNJU-MBWENI DSM WAFARIKI DUNIA.....

Inasemekana watu watatu waliotambuliwa kwa majina ya
Msagala,Jacob na Mhando ambao ni  wakazi wa Bunju jijini
Dar es Salaam wamefariki dunia mchana wa April 04
baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba kokoto.
Watu hao walikua wakichimba kokoto hizo kwenye
machimbo ya Mtanzania mwenye asili ya Kiasia
aliyefahamika kwa jina la Kara Arjan machimbo yaliyopo
eneo la Bunju-Mbweni Dar es salaam.
Taarifa inasema kuwa machimbo hayo yalishapigwa
marufuku kutokana na watendaji wake kufanya kazi katika
mazingira hatarishi ambapo wachimbaji hao wakiwa
kazini,sehemu ya machimbo hayo iliporomoka na
kuwafukia.
Picha za kwenye tukio ambazo zinaonyesha pia juhudi za
watu wakiendelea na uokoaji pamoja ndugu wa waliopoteza maisha


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment