Sunday, April 20, 2014

STORY: BATA MREFU-SEHEMU YA PILI

Story: BATA MREFU
Writter: ALNORD SPORTIEVE
ILIPOISHIA SEHEMU YA 1
Basi ALNORD alimaliza kujiandaa akiwa kavalia nguo zake
alizonunuliwa katika kusherehekea kuvuka mwaka mpya ali
maarufu kama NEW YEAR na kwenda nje ambapo alikua
akisubiriwa na kaka yake huyo...
Alifika pale na kupewa baraka na wazazi wake huku wakimsihi
kua mwaminifu katika biashara ya baba yake mkubwa na pia
kuwa mnyenyekevu na mtiifu pindi awapo nyumbani kwa baba
yake mkubwa....mama ake alimsisitizia sana kuhusu swala la
kujifanya mjinga kwa kila atakachoambiwa na pia kuepuka
kujiingiza katika mapenzi kwani walikua wakisikia kua dar es
salaam kulikua na vishawishi vingi ambavyo vingepelekea
kupata maambukizo ya UKIMWI...walimsihi sana maana
hawakupenda mwanao wa pekee ambao walimpenda kupita
maelezo kwani ndiye waliebarikiwa na MUNGU...
Alnord aliahidi kuyazingatia hayo kisha wakaagana na huku
wazazi wake wakimpa mikono ya kheri kuashiria kua wanamtakia
safari njema..
ENDELEA
Safari ilianza ambapo walienda kwenye stand ndogo ya pale
MFUMBI ili kuvizia mabasi yatokayo MBEYA maana pale hapakua
na stand kubwa kusema kwamba wangekata ticket ofisin..hasa
ukizingatia kile ni kijiji kidogo sana...
Walisubiri sana pale,baada ya kusimamisha mengi yao bila
mafanikio hatimae mnamo saa mbili kamili walifanikiwa
kupanda bus(ABOOD) ndipo safari ikaanza rasmi..walikata ticket
dakika chache baada ya kuingia ndani ya bus hilo...safari yao
haikua nzuri kiasi kwa upande wa ALNORD maana dereva alikua
akiendesha kwa mwendo kasi kidogo kitu kilichomfanya
ALNORD awe mwoga kwani hakuwahi kupanda mabasi makubwa
zaidi ya daladala na coaster ambapo ilikua nadra pia..aliweza
kupanda magari hayo madogo ya abiria iwapo yeye,mama yake
na baba yake wanaenda LEMBUKA(MNADANI) kununua mahitaji
hasa kipindi ambacho sikukuu zinakaribia,kama tunavyojua
watu wengi hupenda kuvaa nguo mpya kila sikukuu kama
mwanafunzi apendavyo uniform mpya ikiwa ni pamoja na
mahitaji yake yote ya shule pindi shule zinapofungua....
*************
""Marry mwanangu,najua ni kipindi kigum kwako..ila usikate
tamaa mwanangu kwani ni moja ya matokeo...chukulia kama
changamoto na inakubid ukabiliane nayo na sio kumwaga
michoz kwan hata ukijaza jaba huwez kubadilisha
matokeo...kufeli shulen sio kufeli maisha...""
Ilikua ni baba ake MARIA C. NGWILLA akimpa moyo mwanae
baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka na kuonesha kua
mwanae MARIA amepata div. 4 ya alama 38 kitu ambacho
kilimfanya mwanae awe mtu wa kulia tu...ndipo akaamua
kumuita na kumpa moyo...
""Lakin baba we mwenyewe unajua jinc gan nilikua nna uwezo
darasan halafu mwishon matokeo yanatoka kama haya kwel
unadhan mi najickiaje?? Hasa ukizingatia huyu mke uliemuoa
baada ya mama kufa anavoninyanyasa hapa nyumban...ntakuaje
na furaha...yan kila cku ananiambia mimi nishinde apo grocery
niuze halafu mwisho wa siku anasema mi namuibia!!! Mi baba
nimechoka bora niende kukaa kwaakina ESTER tu..""
MARRY alimjibu baba ake maneno mfululizo yenye ukweli ndani
yake kwa sauti ya huzuni iliyoambatana na kilio cha kwiwi
ambayo yalionyesha taswira ya maisha ya tabu alioishi MARRY
pale nyumban kwao baada ya MAMA yake mzazi kufa na baba
yake kuoa mke mwingine ambae kiukweli alikua akimnyanyasa
mtoto huyu amba alitoka kuhitimu kidato cha nne katika shule
ya sekondari EDUCARE ndipo akarudi kwao ambako akakutana
na maisha yale ya shuruba...huku akisisitiza kwenda kukaa kwa
rafiki yake ambae walisoma nae shuleni huko na kua marafiki
wakubwa kiasi kwamba alikua na uwezo wa kwenda kukaa huko
bila kipingamizi kutoka kwa wazazi wa ESTER...
Baba yake alihuzunika sana hadi akafikia hatua ya kutoa machozi
kutokana na maneno yaliomuumiza haswa...ndipo akaona ni
bora amhamishe mwanae na kumpeleka DAR ES SALAAM
ambako kuna nyumba alioacha mkewe ili akaisimamie huku
yeye akikaa nyumba ya ndani na pesa ya wapangaji aitumie
kufanyia kitu kitakachomjengea maisha mazuri...
Walikubaliana na mwanae huyo wa mwisho kati ya wanne
ambao ni wakike wawili na wa kiume wawili... mipango ya safari
ilianza...
******
...safari iliendelea huku CHUMA akimuonesha mdogo wake
huyo mshamba kila kituo walichopita ikiwemo
MAKAMBAKO,IRINGA,RUAHA MBUYUNI hadi waliposimama
katika hotel ya ALJAZEERA ili kupata chakula cha mchana...
Walishuka na kwenda kununua chakula huku ALNORD
akishangaa sana mazingira ya hotel ile ikiwa ni pamoja na
vyakula vizuri...
Walirud kwenye gari had mda wa kuendelea na safari ulipofika
na dereva akakanyaga gear.. #vuuuuuuum wakaianza mikumi
ambapo ALNORD alidhihirisha wazi kua yeye ni mshamba
maana alishangaa huku akipiga kelele kwa saut kumuuliza kaka
ake sehemu ile ni nin had alipoambiwa kua ni HIFADHI YA
MBUGA YA WANYAMA hapo angalau alitulia...
Walipita chalinze,morogoro,kibaha hatimaye wakaingia UBUNGO
BUS TERMINAL ambapo ALNORD ndio alichanganyikiwa kabisa
kwani aliyaona majengo makubwa(maghorofa) ambayo alikua
akiyaona kwenye TV tu kule kijijini kwao kwenye mabanda ya
video...
Alihamaki sana had ilibak kidogo agongwe na gari pind
walivokua wanavuka barabara ndipo CHUMA akaona ni bora
achukue tax maana hali ile ilionyesha wazi kabisa kua angeweza
kupata aibu mjini pale...ndani ya lisaa limoja na nusu walifika
nyumban kwa baba ake mkubwa(MR. ABDALLAH
CHUMA)...ambapo alipokelewa kwa furaha sana...na wakampa
mizigo HOUSE GIRL wa pale nyumban...nae akaketi seblen
akisubiri nin kinafuata
#ITAENDELEA panapo majaaliwa


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment