Sunday, April 6, 2014

BABA AMTESA MWANAE KISA HAPENDI WATOTO WA KIUME...

Mtoto Amos Baya mwenye umri wa miaka minne ambaye
toka kuzaliwa kwake amekuwa akipata mateso kutoka
kwa baba yake kisa kwanini kazaliwa wa kiume,hali
iliyosababisha mtoto huyo kudhoofika mwili na kupata
ugonjwa wa utapiamlo Vidole vya mtoto Amos Baya vinavyoonekana hapo
vimevunjwa haviwezi kunyooka Wakati watu wengine wanakesha kutafuta watoto lakini
pia wadau mbalimbali wakiendelea kupiga vita ukatili dhidi
ya watoto,vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea
kujitokeza katika jamii ambapo huko katika kijiji cha
Senane wilayani Maswa mkoa mpya wa Simiyu mwanamme
mmjoa aitwaye Baya  Seni amekuwa akimpa mateso makali
mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka minne ili afe
kwa madai kuwa hapendi watoto wa kiume.
Baya Seni ambaye ni mkazi wa kijiji hicho cha Senane
amekuwa akimpa mateso makali mtoto huyo anayejulikana
kwa jina la Amos Baya mwenye umri wa miaka minne toka
kuzaliwa kwake hali  iliyoelezwa kusababisha mtoto huyo
kudhoofika mwili na kupata ugonjwa wa utapiamlo.
Miongoni mwa mateso aliyoyapata mtoto huyo ni pamoja
na kuvunjwa vidole vya mkono wa kushoto, kutelekezwa
shambani siku zaidi ya mbili bila kula na kuning'inizwa juu
ya mti.
Imeelezwa kuwa Mwanamme huyo hapendi watoto wa
kiume kwa madai kuwa wanaleta umaskini kwa sababu
wakikua watataka kuoa na kuchukua mali, lakini mtoto wa
kike akikua ataolewa na kuleta mali nyumbani.
Taarifa za mtoto huyo kupata mateso kutoka kwa baba
yake mzazi zilitolewa na msamaria mwema   siku ya tarehe
31 mwezi Machi mwaka huu  ambaye alikwenda katika
shughuli za mazishi katika kijiji hicho na kumwona mtoto
huyo ndipo akapiga simu ofisi ya ustawi wa jamii wilaya ya
Maswa na kufuatia taarifa hizo ofisi hiyo iliwataarifu polisi
na wakaenda kumchukua mtoto huyo na kumuweka chini
ya ulinzi baba mzazi wa mtoto huyo.
Afisa ustawi wa jamii wilayani maswa Bwana Husein
Mshana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
Hivi sasa mtoto huyo amelazwa wodi namba nane ya
watoto katika hospitali ya wilaya ya Maswa akipatiwa
matibabu.
Mama mzazi wa mtoto huyo  Elizabeth Paul amekiri kuwa
mtoto huyo amekuwa akifanyiwa vitendo vya ukatili na
baba yake mzazi na kwamba hata yeye  amekuwa akipewa
vitisho kuwa endapo atasema atauawa.
Tayari baba mzazi wa mtoto huyo Amos Baya anashikiliwa
na jeshi la polisi wilayani maswa kwa hatua za kisheria.


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment