Tuesday, September 16, 2014

DR. REGNALD MENGI AINGIA KWENYE TUZO ZA MFANYA BIASHARA BORA AFRIKA MASHARIKI

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk.
Reginald Mengi, ni miongoni mwa
wafanyabiashara wanne waliofikia
fainali ya kuwania Tuzo ya Mwaka ya
Mfanyabiashara Bora Afrika (AABLA)
kundi la Afrika Mashariki.
Sherehe za tuzo za AABLA, kundi la
Afrika Mashariki zitafanyika Septemba
20, mjini Nairobi na zitarushwa
hewani na runinga barani Afrika.
Kwa mujibu wa chaneli ya televisheni
ya masuala ya fedha na biashara
Afrika (CNBC Africa), ambao ndiyo
waandaaji wa sherehe hizo, tuzo hizo
za kila mwaka zimebuniwa kwa ajili
ya kutambua utendaji uliotukuka
katika biashara, wenye mafanikio
makubwa kwenye sekta zao za
biashara na vilevile kwenye jamii
ambapo biashara hizo zinaendeshwa.
“Tuzo hizo ni kutambua uongozi wa
watu hao katika kubadilisha sekta ya
biashara kwa kuendeleza ubora wa
shughuli zao kwa kuzingatia desturi
njema za kufanyabiashara na
ubunifu.”
“CNBC Africa inajivunia kuendeleza
utamaduni uliowekwa na tuzo hizi
unaotambua na kusherehekea
mtazamo, msukumo wa mafanikio na
ubora mkubwa wa viongozi
wafanyabiashara katika bara la Afrika.
AABLA iinawatambua kipekee na
kuwaheshimu viongozi ambao
wamechangia katika kuboresha
uchumi wa Afrika na waelekezi wa
biashara zinazoongoza wakati wa
sasa.
Washindi wa tuzo hizi ni mfano mzuri
zaidi katika uongozi Afrika. Wao ni
uthibitisho wa thamani halisi wa
kiongozi aliyefanikiwa, - mafanikio,
nguvu, ubunifu, ustadi, ujuzi na
uwezo wa kuona mbali thamani
ambazo ni muhimu katika kuunda
biashara kubwa katika uchumi wa
Afrika na ulimwengu.
AABLA ni tuzo moja kubwa zaidi ya
biashara barani Afrika na hutolewa
katika kanda za Afrika Magharibi,
Afrika Mashariki na Kusini mwa
Afrika.
Wafanyabiashara wengine watatu
wateule wa tuzo hiyo ni Ofisa
Mtendaji wa BRITAM, Benson Wairegi,
(Kenya), Ofisa Mtendaji wa CENTUM,
James Mworia, (Kenya) na Ofisa
Mtendaji wa CROWN PAINTS, Rakesh
Rao (Kenya).
Watanzania wengine walioteuliwa
katika tuzo hizo kwa makundi tofauti
ni Ofisa Mtendaji wa Helvetic Solar
Ltd, Patrick Ngowi, (EA Young
Business Leader) na Ofisa Mtendaji
wa Techno Brain Ltd, Manoj Shanker,
(Entrepreneur of the Year).

No comments:

Post a Comment