Thursday, September 25, 2014

ZITTO KABWE KUWAPATANISHA DIAMOND NA ALI KIBA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema), Zitto Kabwe, amejitosa
kusuluhisha ugomvi wa muda mrefu
wa wasanii wawili wa muziki wa
kizazi kipya nchini, Ali Kiba na
Nasibu Abdul 'Diamond'.
Zitto alitoa kauli hiyo juzi wakati
akihojiwa katika Kipindi cha Mkasi
kinachorushwa na Kituo cha
Televisheni cha EATV baada ya
kuulizwa kuwa ni jitihada gani
amezifanya kusuluhisha ugomvi wa
wasanii hao akiwa kama mlezi wa
wasanii wanaotoka mkoani Kigoma.
Alisema anafahamu kuwapo kwa
ugomvi wa kutoelewana kati ya
wasanii Ali Kiba na Diamond na
kwamba alishawahi kufanya jitihada
za kuwaita kila mmoja kwa nyakati
tofauti.
Alifafanua kuwa katika kuhakikisha
anawasuluhisha wasanii hao,
anaifanya kazi hiyo kwa umakini kwa
sababu hataki kuonekana anaingilia
maisha ya watu na kwamba ana imani
atafanikiwa kuwapatanisha.
Kuhusu madai kwamba ana uhusiano
wa kimapenzi na msanii Mwasiti
Almas, alisema ni kweli kumekuwapo
na uvumi huo lakini kimsingi hana
uhusiano wowote wa kimapenzi na
msanii huyo.
"Nasikitishwa na madai hayo
yanayotolewa na baadhi ya watu,
Mwasiti ni kama dada yangu ambaye
nimekuwa nikimsaidia katika kazi
zake, kuhusishwa naye kimapenzi ni
jambo linalonisononesha,"alisema.
Zitto alisema wanaomhusisha katika
suala la mapenzi na msanii huyo ni
kwa sababu Mwasiti ameimba wimbo
ambao amemtaja yeye (Zitto) lakini
kiukweli hana uhusiani naye wa
kimapenzi.
Alipoulizwa ni lini ataoa, alisema
bado 'yupo yupo' na kwamba kuna
mwanamke aliyemtaja kwa jina la
Jack ambaye amezaa naye mtoto
ambaye kwa sasa miaka nane na
anasoma darasa la pili nchini Uganda.
KAMPUNI YA LEKA DUTIGITE
Kuhusu Leka Dutigite inayounganisha
wasanii wa Kigoma All Stars, alisema
ni kampuni ambayo kila msanii
anayetoka mkoani Kigoma ana hisa
na ikipata faida wanagawana.
Zitto alisema Leka Dutigite pia
inamiliki kampuni nyingine ambayo
imekuwa ikipata kazi mfano katika
Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) na
yeye kama mlezi amekuwa akitoa
fedha zake kusaidia.

No comments:

Post a Comment