Wednesday, September 24, 2014

MAGOLI 18 LIGI KUU YASHINDWA KUVUJA REKODI

Magoli 18 yamefungwa kwenye mechi
saba za ufunguzi wa Ligi Kuu
Tanzania Bara iliyoanza Jumamosi
iliyopita, lakini yameshindwa kuvunja
rekodi ya magoli ya msimu uliopita.
Kwenye mechi za ufunguzi wa Ligi
Kuu msimu uliopita jumla ya magoli
19 yalipatikana.
Ligi ya msimu huu imeanza kwa Azam
FC kuitandika Polisi ya Morogoro
mabao 3-1, Mtibwa Sugar kuichapa
Yanga mabao 2-0, Stand United ya
kutandikwa nyumbani mabao 4-1
dhidi ya Ndanda FC kutoka Mtwara,
wakati Mgambo JKT ya Tanga
iliifunga Kagera Sugar bao 1-0.
Mechi nyingine ilikuwa ni Ruvu
Shooting kupata kipigo nyumbani cha
mabao 2-0 kutoka kwa Prisons ya
Mbeya, Mbeya City kulazimishwa sare
ya bila kufungana dhidi ya JKT Ruvu,
huku Simba ikibanwa mbavu katika
sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union,
hivyo kuzaa mabao 18.
Magoli 19 ya mechi ya ufunguzi
msimu uliopita kwa mujibu wa
kumbukumbu zetu yalipatikana kwa
Yanga kuinyuka Ashanti mabao 5-1,
Mtibwa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi
ya Azam, JKT Oljoro ikainyuka
Coastal Union mabao 2-0, Mgambo
ikachapwa 2-0 dhidi ya JKT Ruvu,
Simba ikatoka sare ya mabao 2-2
dhidi ya Rhino ya Tabora, Mbeya City
ikatoka sare ya bila kufungana dhidi
ya Kagera Sugar na Ruvu Shooting
ikaitandaika Prisons mabao 3-0.
Katika hatua nyingine, mchezaji wa
Mgambo Shooting Ramadhani Pera
ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa
kwanza kufunga bao kwenye Ligi kuu
alipofunga bao pekee dhidi ya Kagera
Sugar katika dakika ya 12 kwenye
raundi ya kwanza ya ligi hiyo
Jumamosi.
Mabao yote yaliyopatikana kwenye
mechi nyingine yalifungwa baada ya
dakika hizo.
Shaaban Kisiga wa Simba anashikilia
rekodi ya kufunga bao la mapema
zaidi katika dakika ya saba dhidi ya
Coastal katika mechi ya kufunga
raundi ya kwanza Jumapili.

No comments:

Post a Comment