Thursday, September 25, 2014

WAREMBO WA MISS TANZANIA WATALII MTO WA MBU

Warembo wanaotarajia kushiriki
shindano la urembo la taifa mwaka
huu "Redd's Miss Tanzania 2014" leo
wanatarajia kutembelea eneo la Mto
wa Mbu kushuhudia maajabu yaliyoko
kwenye mto huo ulioko Karatu
mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya
kufanya utalii wa ndani
Akizungumza na gazeti hili jana kwa
njia ya simu, Ofisa Habari wa Kamati
ya Miss Tanzania, Haidan Rico,
alisema kuwa wakiwa eneo hilo,
warembo walipewa maelezo muhimu
kuhusiana na mto huo na dhumuni la
kuwatembeza warembo hao katika
vivutio mbalimbali ni kutaka
kushawishi jamii kufanya utalii
Rico alisema kuwa wanaamini
warembo hao watafikisha ujumbe
katika familia zao na kubadili mawazo
kwamba utalii ni kwa ajili ya wageni
pekee.
Alisema kuwa kesho Jumanne
warembo hao wataelekea Ngorongoro
Crater kuona jinsi eneo hilo
lilivyobonyea kufuatia mlipuko wa
volkano.
Alisema kuwa tayari warembo hao
wameshatembelea katika lango la
kupanda mlima Kilimanjaro na
kuelezwa mazingira yanayozunguka
eneo hilo, Tarangire na kufanya kazi
za kijamii kwenye hospitali za Kilema
na Marangu ambapo walitoa misaada
ya sabuni, vyandarua, dawa ya meno,
miswaki na mafuta ya kujipaka kwa
watoto na wanawake waliolazwa
kwenye hospitali hizo.
Pia washiriki hao walitembelea
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA) na wakiwa hapo
walijifunza mbinu ambazo askari
wanatumia kukagua abiria ambao
wanasafiri na bidhaa zisizoruhusiwa
kama vile dawa za kulevya.
Pia alisema washiriki watamtembelea
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini na
baadaye Hifadhi ya Mbuga ya Arusha.
Warembo hao 30 kutoka mikoa
mbalimbali nchini ambao wako katika
ziara hiyo ni pamoja na Dorice Mollel,
Sofia Masey, Lilian Timothy, Junes
Ndalima, Maureen Godfrey, Martha
John, Naba Magambo, Raisa Julius,
Happiness Samuel, Evelyn Baasa,
Lilian Kamazima, Elizabeth Tarimo,
Nidah Katunzi, Lucy Diu, Mariam
Hussein, Maria Shilla, Camilla John,
Queen Latifa Hashim na Dorren Beno.
Warembo wengine ni Sitti Mtemvu,
Salama Saleh, Patricia Pontain,
Rachel Clavery, Mary Emmanuel,
Nicole Sarakikya, Dorren Robert,
Jihan Dimachk, Nasreen Abdul,
Sabina Thomas na Happinness
Sosthenes.
Happiness Watimanywa kutoka
mkoani Dodoma ndiye mrembo
anayeshikilia taji hilo la taifa na
baadaye mwaka huu ataiwakilisha
nchi kwenye fainali za urembo za
dunia.

No comments:

Post a Comment