Saturday, September 13, 2014

MAMA NEY WA MITEGO AFUNGUKA HOFU YAKE JUU YA MWANAE

Mama mzazi wa mkali wa bongofleva
Nay wa Mitego ameongea kwa mara
ya kwanza na chanzo chetu na
kusema ana wasiwasi na mwanae
ambae hivi karibuni ametoa video
mpya aliyoifanya nchini Kenya.
Amekiri kweli kwamba siku kadhaa
zilizopita ilibidi amwite na kumuweka
chini Nay wa Mitego akitaka amueleze
kama ni kweli amejiunga na
‘freemason’ ambayo wengi
wanaitafsiri kwamba ni dini ya
kumwabudu shetani kitu ambacho
kiliwahi kukanushwa na aliyewahi
kuwa mmoja wa viongozi wa
freemasons Tanzania.
Mama anasema alimketisha Nay chini
baada ya video ya ‘Mr. Nay’ kutoka
ambapo baadhi ya picha sio za
kawaida mfano damu pamoja na
alama zilizotumika ndani yake.
Amesema ‘Naitwa Matilda Mwaipopo
ni mama mzazi wa Nay, kwakweli
mwanangu namchukulia lakini sifa tu
zinazokuja kama Nay kwenye
magazeti, Nay freemason, watu
wanakuja wananisimamisha….
mwanao Nay kweli? mbona tunasikia
freemason? basi kichwa changu
kinapagawa…. ‘
‘Nikiangalia miziki anayoifanya kama
hii aliyoitoa juzi, jamani mwanangu
anaambiwa freemason usikute kweli
freemason, Nay wa Mitego
nimemuita…. mwanangu vipi?
ninayoambiwa ni ya kweli? Freemason
wewe? mbona wimbo wako huu
siuelewielewi? ananiambia mama
mimi sio freemason, namwambia
hapana mwanangu hapana….. nasikia
freemason watu wanatoaga hata
wazazi sadaka’
‘Mimi ndio mama niliebakia baba
yenu alifariki aliniacha ukiwa na
miaka mitatu nimejitahidi kukulea
mpaka leo…… unitoe sadaka mama
yako kweli?????!!! Nay wa Mitego
sana ni kucheka…… anaona tu mama
kama anapagawa, lakini kwakweli
mwanangu simuaminiamini miziki
yake hii anayoifanya’

No comments:

Post a Comment