Tuesday, September 16, 2014

WANAFUNZI JIJINI DAR WADAI KUA WANATONGOZWA NA WALIMU WAO

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Mwanalugalo, jijini Dar es Salaam,
wamelalamikia uongozi wa shule
kutowaonya baadhi ya walimu wa
kiume wenye tabia ya kuwataka
kimapenzi wanafunzi wa kike.
Wanafunzi hao walitoa malalamiko
hayo wakati wakizungumza na
NIPASHE katika wiki ya ukaguzi wa
shule nchini jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi waliozungumza
kwa masharti ya kutotajwa majina
walisema baadhi ya walimu katika
shule hiyo wamekuwa wakiwataka
kimapenzi wasicha kwa kuwapa ahadi
nyingi ikiwamo kuwalipia usafiri wa
pikipiki kila siku na kuhakikisha
wanafaulu masomo
wanayowafundisha.
“Walimu hapa wanakutonga na
kukuahidi kufaulu, ukiwa mjinga
unakubali, lakini wengi tumewazoea
kazi yao nikutongoza kila mtu,”
alisema mwanafunzi mmoja.
“Ikitokea umekataa kutembea na
mwalimu ujue kama anakufundisha
somo lake darasani atakuchapa
mpaka ukome, lakini inabidi tuvumilie
tu,” alisema mwanafunzi mwingine.
Katika ukaguzi huo uliofanywa na
Mkurugenzi na Mkaguzi Mkuu wa
Shule za Sekondari, Marrystala
Wasena, alisema kitendo hicho ni cha
kinyama na kuahidi kuhakikisha
anawashughulikia walimu wote
watakaohusika kufanya vitendo hivyo.
“Hatuwezi kulivumilia tabia hii
iendelee, ni bora shule ibaki na
walimu wa chache kuliko kuwa na
walimu waiana hii,” alisema.
Akizungumzia tuhuma hizo, mkuu wa
shule hiyo, Aron Ndunguru, alisema
tuhuma hizo hazina ukweli wowote.
“Wanafunzi ni waongo wenyewe
ndiyo wanawatongoza walimu wao ili
watembee nao halafu wanasema wao
ndiyo wanatongozwa,” alisema
Ndunguru.

No comments:

Post a Comment