Thursday, September 25, 2014

WASANII WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KWENYE SIKU YA SANAA

Viongozi wa mashirikisho ya filamu
na sanaa za ufundi wamewataka
wasanii wa fani mbalimbali kujitokeza
katika kushiriki semina
zitakazoendeshwa katika Siku ya
Msanii Tanzania.
Semina ya Siku ya Msanii inatarajiwa
kufanyika Oktoba 22 na 23 mwaka huu
katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere
(Makumbusho Posta) na wasanii
watafundishwa mambo
mbalimbali.Rais wa Shirikisho la
Sanaa za Ufundi, Adrian Nyangamale,
alisema wasanii wanapaswa
kujiandikisha kwenye semina hizo ili
kupata ujuzi wa mambo mbalimbali.
“Semina hizi ni muhimu kwa sababu
kutakuwa na wataalamu kutoka katika
sekta mbalimbali ambao watakuja
kutoa mafunzo kwenye semina hizo,
jambo ambalo litachangia uelewa na
elimu ya wasanii, tumekuwa
tukilalamika kuwa hatupati fursa za
elimu lakini Siku ya Msanii imetupa
hiyo nafasi sasa tuitumie,” alisema.
Naye Makamu wa Rais wa Shirikisho
la Filamu, Selemani Ling’ande alisema
wasanii wajitokeze kwenye semina
hizo lakini pia aliwataka wananchi
kujitokeza kwa wingi katika kupiga
kura za kupata watu watakaowania
tuzo za Siku ya Msanii.
“Semina ni muhimu lakini kuna suala
la kutambulika mchango wa wasanii,
hapa ndiyo Watanzania
wanapotakiwa kufanya mapendekezo
yao, kuna fomu zinatolewa kwenye
magazeti na mitandao juu ya Tuzo za
Humanitarian Award na Life Time
Achievement ambazo wasanii wote
wanaweza kushindanishwa,” alisema.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya
Haak Neel Production, Godfrey Katula,
ambaye kampuni yake ndiyo imepewa
jukumu la kusimamia Siku ya Msanii,
alisema Watanzania wajitokeze
kupendekeza majina ya wasanii
wanaostahili kupata tuzo na Kamati
ya Utafiti itakwenda kuhakiki taarifa
zote zilizowasilishwa kwao.
“Kazi za wasanii zinaanza
kutambulika hapo, wananchi
wanawajua hivyo ni fursa yao
kuonyesha kuthamini kazi zao, lakini
pia tunawataka wasanii wajitokeze
kwenye semina ambazo zitafanyika
kwa siku mbili ili kupata elimu
sahihi,” alisema.
Siku ya Msanii inaandaliwa na
Kampuni ya Haak Neel Production
kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa
la Taifa (BASATA).

No comments:

Post a Comment