Tuesday, September 30, 2014

KURA ZA HAPANA ZAENDELEA KURINDIMA BUNGENI

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,
akipiga kura wakati wa zoezi la
kupigia kura Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa na bunge hilo mjini
Dodoma jana.Picha/ Khalfan Said.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,
jana walianza kupiga kura kupitisha
Rasimu ya Katiba inayopendekezwa,
huku ikifanyika kampeni kali kusaka
theluthi mbili za wajumbe baada ya
suala la Mahakama ya Kadhi
kushindikana kuingizwa kwenye
rasimu hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
wajumbe watatu wanaowakilisha
madherhebu ya dini na Mwenyekiti wa
Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge,
walipewa fursa ya kuzungumza na
kutoa kauli za kuwashawishi wajumbe
wakubali kuipitisha rasimu hiyo huku
suala kubwa likiwa ni Mahakama ya
Kadhi.
KAULI YA PINDA
Kabla ya hatua ya kupiga kura kuanza
jana alasiri, Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, alilazimika kutoa tamko la
serikali kufuatia taarifa kwamba
wajumbe hususan ambao ni waumini
wa dini ya Kiislamu, wamedhamiria
kuipigia kura ya `Hapana' rasimu
hiyo.
Msimamo wa kuipigia kura za
`hapana' rasimu hiyo ulitolewa
mwishoni mwa wiki na baadhi ya
wajumbe kwa nyakati tofauti bungeni
wakati wakihakiki Rasimu ya Tatu
iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa
Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge,
ambayo haijaingiza suala la
Mahakama ya Kadhi kama ambavyo
walitaka iwe.
Akitoa tamko hilo, Waziri Mkuu Pinda,
alisema linafuatia kikao cha
maridhiano cha pamoja kati yake na
Kamati ya Uongozi wa BMK ambacho
pia kiliwashirikisha pia viongozi wa
dini za Kiislamu na Kikristo.
Alisema suala la Mahakama ya Kadhi
ambalo lilianza tangu mwaka 2005,
lilifikia hatua nzuri kwa waumini wa
dini ya kiislamu kuanzisha mahakama
hizo mikoa yote nchini, mwaka
2011/12.
Hata hivyo, alisema tatizo ambalo
limejitokeza kwa sasa ni utekelezaji
wa maamuzi yanayofikiwa kwenye
mahakama hizo kwa upande wa
serikali.
Alisema: “Taifa hili ukiondoa ubaguzi
serikali na kama nchi tumejitahidi
sana kama serikali, tumejitahidi sana
kama nchi kutenganisha shughuli za
imani za dini na shughuli za serikali.”
Alisema huo ndiyo msingi muhimu
sana kwa sababu serikali haina
dini.“Serikali hii haina dini…nchi hii
haina dini, lakini kwa Mtanzania
mmoja mmoja, lazima tuheshimu sana
yale ambayo yeye anaamini kwa imani
yake,” alisema. Alisema kazi ya
serikali ni kuweka mazingira mazuri
ya kuhakikisha kila mmoja anapata
fursa nzuri ya kuamini imani yake.
Alisema nguzo hii muhimu imesaidia
sana kujenga umoja, amani, utulivu
na mshikamano wa taifa hili kwa
kipindi chote hicho na kwamba ni
matarajio ya Katiba mpya nayo italeta
mshikamano huo kwa miaka mingi
ijayo.
“Nawaombeni sana wote katika jambo
hili tusitetereke, tukatae hisia zozote
ambazo zitatuletea uvunjifu wa
amani,” alisema.Alisema baada ya
kikao chao cha Jumamosi, viongozi
hao wa dini waliitaka serikali kutoa
ahadi ni lini sasa wataboresha sheria
zake ili maamuzi yanayotolewa na
mahakama hizo yasiendelee
kupuuzwa yanapopelekwa serikalini.
Pinda alisema kwa kuzingatia
umuhimu huo, serikali itaziangalia
sheria zake mbili ambazo ni Sheria ya
Mahakama ya Mahakimu, Sura yua 11
na Sheria ya Kiislamu, sura ya 375, na
wataleta muswada bungeni ifikapo
Januari mwakani.
Alisema kabla ya kuwasilisha
muswada huo utawashirikisha wadau
wengi na ukifikishwa bungeni
wataangalia namna gani bora ya
kutekeleza maamuzi yao. Anasema
awali alikuwa mbumbumbu sana
katika eneo hilo, lakini baada ya
mazungumzo hayo ameelewa vizuri.
SHEIKH THABIT JONGO
Akizungumza baadaye Mjumbe wa
BMK, ambaye anatoka kundi la 201
(dini), Sheikh Thabit Jongo, alisema
wajumbe bungeni humo wanashukuru
kwa tamko lililotolewa na serikali
kupitia Waziri Mkuu.
“Wajumbe humu ndani wathamini
kauli ile iliyotolewa na Waziri Mkuu…
kitu nyeti na kinachoweza kuvuruga
amani ni suala la imani ya dini mtu.
Humu ndani suala la Mahakama ya
Kadhi lilitaka kutuvuruga,” alisema.
Alisema wapo Waislamu ambao
walikuwa hawaipendi mahakama hiyo
na wapo Wakristo pia ambao hawataki
mahakama hiyo.Lakini kutokana na
tamko lililotolewa na Waziri Mkuu
jana, anawaomba wale wote
waliokuwa na mipango ya kuipigia
kura ya hapana rasimu hiyo sasa
mipango hiyo waifute.
Sheikh Thabit alisema maadui wa
bunge hilo ni watatu ambao ni
kwanza kundi la Umoja wa Katiba ya
Tanzania (Ukawa) ambao wangependa
bunge hilo livunjike.
Alimtaja adui wa pili kuwa ni
aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph
Warioba, ambaye mara kwa mara
amesikika akilipinga bunge hilo na
hata kudai kuwa atakwenda mitaani.
Adui wa tatu kwa mujibu wa Sheikh
Thabit, ilikuwa ni suala la Mahakama
ya Kadhi, lakini kutokana na tamko la
serikali jambo hilo litashughulikiwa
ifikapo Januari mwakani kwa maana
ya kurekebisha sheria ili utekelezaji
wa maamuzi ya mahakama hizo
yaweze kushughulikiwa na serikali.
Sheikh Hamid Jongo
Kwa upande wake, Sheikh Hamid
Masoud Jongo, alisema kwa kuwa
tamko hilo limetolewa na ofisi ya
Waziri Mkuu kwa maana ya taasisi
basi utekelezaji wake usiwe na
kigugumizi tena kesho kutwa.
Alisema Waislamu hawana nia haswa
ya kuvuruga mchakato huo, lakini
akataka ahadi iliyotolewa na Waziri
Mkuu iheshimiwe.
ASKOFU MTETEMELA
Naye Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa
la Anglikana Tanzania, Donald
Mtetemala, alisema suala la
Mahakama ya Kadhi kwa muda mrefu
lilileta wasiwasi kutokana na hofu ya
kusababisha mpasuko kwa jamii ya
Watanzania.
Alisema upo mpasuko wa kisiasa,
lakini mpasuko wa kidini ni mbaya
sana, hivyo ndiyo maana suala hilo
limechukua muda mrefu ili kulipatia
ufumbuzi.
“Nimeona roho ya kuvumiliana,
ukomavu katika tamko la Waziri Mkuu
Pinda. Alisema rasimu hiyo ina suala
la msingi kwamba serikali na nchi hii
kwa ujumla haina dini.Aliwaomba
waumini wa dini ya Kikristo kuelewa
suala hilo kwa mapana yake.
CHENGE
Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya
Uandishi, Andrew Chenge,
akiwasilisha marekebisho ya Rasimu
ya Katiba inayopendekezwa alisema
rasimu hiyo imefuta na kuandika upya
Ibara ya 2(2) ambayo sasa itakuwa
ikisomeka kuwa, “Rais wa Jamhuri ya
Muungano atakuwa na mamlaka ya
kuigawa Jamhuri katika mikoa, wilaya
na maeneo mengine:
Alisema: “Isipokuwa kwa upande wa
Tanzania Bara, Rais atashauriana na
Rais wa Zanzibar kabla ya kuigawa
Tanzania Zanzibar katika mikoa,
wilaya au maeneo mengine.”
Kabla ya marekebisho hayo, rasimu
yake aliyoiwasilisha wiki iliyopita,
ilisema kwamba Rais wa Jamhuri
angekuwa na mamlaka ya kuigawa
mikoa, wilaya Tanzania Zanzibar,
lakini bila kushauriana na Rais wa
Zanzibar.
Aidha, alitaja marekebisho mengine
kuwa ni kuongeza Ibara mpya ya 44A
inayozungumzia Haki za wakulima,
wafugaji, wavuvi na wachimbaji
madini.
Pia, alisema rasimu imeongeza Ibara
mpya 48A kuhusu Haki ya afya na
maji safi na salama na Ibara ya 55
imefanyiwa marekebisho na kuweka
haki kwa wazee.Alisema Ibara
nyingine iliyoongezwa ni ya 100A
inayohusu Makamu wa Kwanza wa
Rais kushindwa kumudu majukumu
yake.
Kuhusu idadi ya mawaziri alisema
rasimu imeweka ukomo kwamba sasa
imeweka idadi ya mawaziri na
manaibu wao wasizidi 40.
Alisema rasimu pia imeunda Tume ya
Uratibu na Uhusiano ya Muungano
ambayo itakuwa ikishughulika na
usuluhishi wa migogoro kati ya pande
mbili za Muungano kabla ya kufikisha
migogoro hiyo Mahakama ya Juu.
Ibara nyingine mpya ni 208A ambaye
inazungumzia Tume za Kisekta
ambayo itakuwa na tume mbalimbali
za huduma. Kadhalika, alisema
rasimu imeongeza ibara nyingine
mpya 242 kuhusu Udhibiti wa rushwa.
UPIGAJI WA KURA
Zoezi la upigaji kura lilianza kwa
kusuasua baada ya baadhi ya
wajumbe hasa wa kutokea upande wa
Zanzibar, kuikataa kwa kupiga kura za
wazi.
Hatua ya baadhi ya wajumbe kutoka
Zanzibar kupiga kura ya hapana,
ilitarajiwa kutokana na msimamo wao
wa awali waliouonyesha baada ya
suala la Mahakama ya Kadhi
kutoingizwa kwenye Rasimu hiyo.
Wajumbe hao bila woga walipiga kura
ya wazi na kutamka kuwa hawaungi
mkono ibara zote za Rasimu hiyo.
Hata hivyo, wapo baadhi ya

No comments:

Post a Comment